Auric

Jumapili, 1 Desemba 2013

News Alert: Mabasi sita ya abood yashikiliwa kwa kuzidisha uzito mizani ya kibaha usiku huu

Habari zilizotufikia muda huu ni kwamba Abiria wa mabasi sita ya Abood wamebaki njia panda baada ya magari waliokuwa wakisafiria kuzuiliwa kwenye mizani ya ya kibaha baada ya kuzidisha uzito. Endelea kufuatilia kwa taarifa zaidi hapa

Ijumaa, 22 Novemba 2013

MKEKA WA NGUVU KUTOKA WILAYA YA NAMTUMBO KUELEKEA WILAYANI MBIGA MKOA WA RUVUMA







Jumapili, 27 Oktoba 2013

Picha: Tembo mwenye hasira, amtembezea kichapo kikali mnyama kiboko

Ndo hapa ukisikia kiboko kachwapwa viboko, tembo alieonekana kuwa na hasira amekamatwa kwenye kamera akitoa kipigo cha mbwa mwizi kwa kiboko.

Kiboko huyo aliyekuwa na mtoto wake pamoja na kiboko mwingine aliingia kwenye 18 za tembo kwenye hifadhi ya Erindi Private Game Park nchini Namibia na kugalagazwa vibaya.

Shuhudia tukio zima katika picha
hippo-and-elephant
hippo-verse-elephanthippo-and-elephant-fightChanzo: Geographic

Ziwa Manyara lipo hatarini kutoweka kabisa kama juhudi hazitachukuliwa kutunza Mazingira

04 (1)
Mahmoud Ahmad  Arusha
Mkutano wa siku mbili wa kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Arusha (RCC) Umeelezwa kwamba Ziwa Manyara (pichani) lipo hatari ya kutoweka kabisa kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo uharibifu wa mazingira unakotokana na Kilimo pembezoni mwa mito kama juhudi za makusudi hazikuchulia kutunza mazingira yanayozunguka maeneo ya mito mbalimbali inayoingia ziwani humo.
Hali hii imetokana na kuongezeka kwa shughuli za kibianadamu hussani za kiuchumi na kusababisha pia Ziwa Manyara kujaa udongo na matope pamoja  uharibifu mkubwa wa mazingira.
Akiwasilisha mada kuhusu changamoto za uhifadhi katika hifadhi ya ziwa Manyara,Muikolojia katika hifadhi hiyo Bi. Christina Kiwanga amesema kukosekana kwa utashi wa kisiasa ni changamoto kubwa katika kuliokoa ziwa hilo.
Bibi Kiwanga ametaja changamoto nyingine ni pamoja na kukosekana kwa mipango endelevu katika baadhi ya vijiji kuhusu umuhimu wa uhifadhi sanjari na elimu.
Muikolojia  huyo amewambia wajumbe wa kamati ya Ushauri ya Mkoa  wa Arusha kwamba shughuli za Biandamu hususani za Kilimo na za kiuchumi zimechangia kwa kiwango kikubwa  hifadhi hiyo kuwa katika hatari ya kutoweka.
Naye Meneja Ujirani Mwema makao makuu ya TANAPA Bw. Ahmed Mbugi amesema  umuhimu wa maeneo ya Mapito ya (SHOROBA) na mitawanyiko ya wanyama katika hifadhi amesema asilimia 80 ya Shoroba  zilizokuwepo miaka ya nyuma zimetoweka kabisa.
Amesisitiza kwamba ni lazima  wananchi  walinde  uasilia  wa mapito ya  wanyama pori kutokana na umuhimu wa maeneo hayo
Mbungi amefafanua kwamba awali kulikuwa na  Maeneo ya SHOROBA yenye ukubwa  wa ekari 40,000 katika hifadhi za Arusha Kilimanjaro, Manyara lakini maeneo haya yamepungua.
Aidha amesisitiza kwamba wanasiasa wanachangia kuhujumu maeneo haya ya uhifadhi kutokana na kukosekana  kwa kuchukuwa maamuzi mazito ya kuyalinda maeneo hayo kwa kuogopa wapiga kura hali inayoleta changamoto mbalimbali pindi wanapotoa taarifa za kulinda maeneo hayo.
Pia ameeleza kwamba asilimia 70 ya mapato yanayotokana na uhifadhi  yanatumika  katika kusajidia  utekelezaji wa miradi ya kijamii ikiwemo ya Afya,Elimu, Maji, na miradi ya Barabara.
Amesema migongano baina ya wanyamapori na  binadamu inachangiwa na binadamu kuingilia maeneo ya mapito ya wanyamapori hivyo kuwakosesha njia za kupita hali inayoharibu mazingira.
Amesisitiza kwamba  hatua hii inasababisha kuathiri shughuli za utalii ambapo idadi ya watalii hupungua sanjari na shughuli za  Uchumi kuathirika Mbali na hali hii katika kipindi cha mwaka  1957/63 na 1987/`988 uoto wa asilimia   hususani misitu ulipungua kwa asilimia 13.5 wakati  maeneo ya kilimo yaliongezeka  kwa asilimia 10.9.
Aidha  maeneo ya ushorobo yaliyotumika kwa  shughuli za kilimo kati ya mwaka 1997/98 yaliongezeka  kati ya asilimia  8.35 hadi 11.41.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Lazaro Maasae yeye amesema kasi  ya ziwa mmnyara kuendelea kujaa ugondo na matope ni ya kasi zaidi.
Chanzo: Moblog

Jumatatu, 23 Septemba 2013

Introducing to you 'My Trip Travel & Tours'

I would like to introduce My Trip Travel & Tours LTD a recently established company in Dar es Salaam, Tanzania. We have an excellent team of highly experienced, motivated and dedicated staff.

We will be delighted to help you with any future travel plans you may have, whether it is a cruise, a holiday package, wildlife safaris, honeymoon packages, adventure holiday, your flights, or a short break— whatever you are looking for, we are here and ready to help.


As a comprehensive travel agency, we are the agent for all Local and International Flights. We book online and issue you with an Electronic Ticket.

If you have been looking or booking online recently, please give us a call before you do so again, as a company we do offer services that are of the highest standard and at extremely competitive rates — and this can be done over the telephone or by email. You will also be able to use our staff’s knowledge to help you find the perfect holiday.

We hope you will support My Trip Travel & Tours LTD and give us a call on +255 688 002000/ +255 776 944 444, email toinfo@mytriptraveltz.com, or drop in to our office at Royal Mirage Hotel Building, Ground Floor at Living stone/Amani Street tosee us.
We are looking forward to assisting you and hope you will contact us in case you need to utilize any of the services and expertise that our company provides.


We guarantee you high quality service.

Picha sita za muonekano wa jengo jipya la uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) baada ya ujenzi kukamilika

Harakati za maandalizi ya ujenzi wa jengo jipya (Terminal 3) la uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), zimekuwa zikiendelea polepole hali inayowatia shaka wadau wengi wa sekta hii ya usafiri wa anga. Kuanza kwa ujenzi wa jengo hilo ni jambo linalosubiriwa kwa hamu kubwa na wadau wa sekta ya usafiri wa anga kwani kukamilika kwa jengo hilo kunategemewa kuleta mabadiliko makubwa sana katika huduma zitolewazo na kuleta ufanisi mkubwa katika huduma za usafiri wa anga na hatimae kukuza uchumi wa nchi.

Hivi karibuni wataalamu na mafundi wa kampuni iliyopewa zabuni ya kujenga jengo hilo, kampuni ya BAM ya Uholanzi, walionekana wakifanya maandalizi ya mwanzo ya ujenzi huo ikiwa ni pamoja na kuzungushia uzio baadhi ya maeneo, upimaji wa ardhi na kubandika michoro yenye kuonesha jinsi taswira ya jengo hilo itakavyokuwa.

Mtandao wa Aviationtz umeshare picha zifuatazo zikionyesha maeneo mbalimbali ya jengo hilo pamoja njia za ndege.

Huu ni muonekano kwa upande wa nje ya jengo na nje ya uwanja.

Hapa ni mahali ambapo abiria watakuwa wakisubiri kabla ya kwenda kupanda ndege (Departure Lounge)
Muonekano wa ndani ya jengo

Jinsi patakavyoonekana kutokea angani

Muonekano wa jengo,njia za ndege na maegesho ya magari.

Upande wa maegesho ya ndege
Ujenzi wa jengo hilo umepangwa kufanyika kwa awamu mbili. Kukamilika kwa awamu ya kwanza kutawezesha uwanja huo kufikia uwezo wa abiria mil 3.5 kwa mwaka tofauti na jengo la sasa ambalo uwezo wake ni abiria mil 1.5 kwa mwaka. Awamu ya pili itaongeza uwezo huo hadi kufikia abiria mil 6 kwa mwaka. Baada ya kukamilika jengo hilo, jengo lililopo sasa (Terminal II) litatumika kwa shughuli za abiria wanaosafiri ndani ya Tanzania tu.

Chanzo: Aviationtz